Sekta Ya Madini Kufungamanishwa Na Mipango Ya Taifa Uwekezaji

 

Wizara ya Madini imeweka  Mipango ya kuhakikisha Sekta ya  Madini inafungamanishwa na mipango ya taifa ili kuwa na Matumizi yenye tija katika rasilimali za nchi hususan katika Sekta ya Madini.


Hayo yamesemwa leo Oktoba 4, 2023 Jijini dodoma na Waziri wa Madini Mhe. Anthony  Mavunde alipokutana  na Waziri Ofisi ya Rais Uwekezaji na Mipango Prof. Kitila Mkumbo wakati wa kikao kifupi kilicholenga kujenga mahusiano mazuri ya uwekezaji nchini Ofisi za Wizara ya Madini.


Amesema ushirikiano wa Wizara hizo mbili utaimarishwa ili Sekta ya Madini iweze kuingizwa katika mipango yenye tija kwa taifa na hatimaye kukuza uchumi wa madini.


Mhe. Mavunde amesisitiza kuwa madini ni sayansi hivyo Sekta ya Madini itahakikisha inafanya utafiti wa madini nchini kupitia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ili kuvutia wawekezaji nchini.


"Lazima tupate taarifa sahihi za madini yaliyopo nchini hususan kwenye mahitaji makubwa ya madini muhimu na madini mkakati ili madini hayo tuyachimbe kwa kiasi kikubwa nchini," amesema  Mavunde.


Hata Hivyo kwa  upande wake Prof. Kitila Mkumbo ,amesema Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji inaratibu na kuweka mazingira mazuri yanayoratibika kwa uwekezaji katika Taasisi za Umma


 Prof. Kitila "mahitaji ya madini hayo duniani iwe chachu kwa Tanzania kutumia fursa hiyo katika kujenga mazingira bora ya kiuchumi ikiwa pamoja na kuibua maeneo


Pia, Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Madini Angelo Haule amesema mapendekezo ya Vipaumbele kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 ni kuendelea kufanya utafiti wa jiofizikia kwa kutumia ndege (High Resolution Airborne Geophysical Survey) na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji maduhuli na utoaji wa leseni.


"Tutaimarisha uwekezaji na Teknolojia katika Sekta ya Madini ili kuendeleza madini muhimu na madini mkakati katika kuhamasisha uwekezaji, biashara na uongezaji thamani Madini,"  Haule.

Post a Comment

Previous Post Next Post