Neema ya Maji Dodoma Bwawa la Farkwa Kuanza Kujengwa

Wizara ya Maji imesaini Mkataba wa mwaka mmoja na Kampuni ya SU-YAPI Engineering Consulting Inc. kwa ajili ya kufanya kazi ya usanifu wa Ujenzi wa Bwawa la Farkwa litakalojengwa katika Wilaya ya Chemba, ambalo litanufanisha wakazi wa Wilaya za Chemba, Chamwino,Bahi na Jiji la Dodoma.

Mkataba umesainiwa leo tarehe 23 Oktoba, ikiwa ni awamu ya kwanza, mradi ambao utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 312 kwa ujenzi wa Bwawa lenye ujazo wa lita za maji milioni 440.

1000360228
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ameshuhudia Hafla hiyo na amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kiasi cha shilingi bilioni 312 ili kuondosha tatizo la maji katika Wilaya nne za Mkoa wa Dodoma ili wakazi wake wapate majisafi, salama na yenye kutosheleza


Post a Comment

Previous Post Next Post