NaPaul Kayanda
Paul Makonda Aibukia CCM
ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaamkipindi cha serikali ya awamu ya Tano chini ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Paul Makonda ameteuliwa kuwa katibu wa itikadi na uenezi kuchukua nafasi
ya Sofia Eduard Mjema ambaye ameteuliwa kuwa mshauri wa Rais masuala ya wanawake,watoto na makundi maalumu.
Ndivyo ninavyoweza kusema baada ya Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana leo Octoba 22,2023 Jijini Dodoma katika kikao chake maalumu chini ya mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na masuala mengine ambapo kimefanya mabadiliko ya Sekretalieti ya Halmashauri kuu ya Taifa kwa kumteua Makonda kuwa katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Itikadi na uenezi kuziba nafasi ya mtangulizi wake Sofia Mjema.
Pamoja na mambo mengine Mjema naye ameteuliwa kuwa mshauri wa Rais Masuala ya wanawake, watoto na makundi maalumu.
Kikao hicho cha Halmashauri kuu ya CCM Taifa pia imelidhia kwa kauli moja na kuielekeza Serikali kuendelea na hatua ya utiaji saini mikataba ya uendlezaji na uwekezaji wa bandari.
Pia Halmashauri kuu ya CCM Tafa imemteua ndugu Rabia Abdalah Hamidu kuwa katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa, Siasa na uhusiano wa kimataifa (SUKI) akichukua nafasi ya ndugu balozi Mbaruku Nassoro Mbaruku ambaye ni Naibu Waziri wa Africa mashariki.
Kufuatia hali hiyo Katika kikao hicho Halmashauri kuu ya CCM Tafa imezipongeza Serikali zake mbili Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibari chini ya Dkt. Hussein Ally Mwinyi ambaye pia ndiye mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Za

Post a Comment