Makamu Wa Raisi Katika Jukwaa La NGO's 2023

DODOMA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. PhilipMpango ametoa wito kwa mashirika yasiyo ya kiserikali nchini (NGO’s)kuwajibika kutunza na kulinda maadili kwa kuheshimu mila, desturi natamaduni za kitanzania wakati wa utekelezaji wa programu mbalimbali.

Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akifunga Jukwaa la Tatu la Mwakala Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) llililofanyika katika Ukumbi waMikutano wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma. Aidha amewataka kuzingatiasheria za nchi na kufuata miongozo mbalimbali inayoratibu shughuli zamashirika hayo.

Makamu wa Rais ametoa rai kwa NGO’s kuhakikisha hazitumiki kuharibumaadili ya Tanzania kwa kutekeleza ajenda binafsi zisizofaa. Ametoa wito kwaKamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Ustawi na Maendeleo ya Jamiikufanya uchambuzi makini wa mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nakuishauri serikali ipasavyo juu mwenendo na ufanisi wa mashirika hayo.

Pia Makamu wa Rais amesema suala la mabadiliko ya tabianchi linapaswakuchukuliwa kwa umuhimu mkubwa na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwaniTanzania ni miongoni mwa nchi zilizoathiriwa na mabadiliko ya tabianchi nahali ya hewa isiyotabirika.

 Amesema serikali Serikali ingependa kuona ushiriki zaidi wa NGOs katika utoaji elimu na hamasa kuhusu uhifadhi wa mazingira,udhibiti wa majanga na maisha endelevu, utunzaji wa misitu na uoto wa asilina kuchangia katika utengenezaji au uboreshaji wa sera mbalimbali. 

Aidhaamesema mashirika hayo yana nafasi ya kubuni programu muhimu kamaukusanyaji na urejelezaji taka, biashara ya kaboni, uanzishwaji na utunzaji wavitalu vya miti na usambazaji wa miche pamoja na usafi wa mazingira katikamaeneo maalum.

Kwa Upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake naMakundi Maalum Dkt. Doroth Gwajima amesema NGO’s zimekuwa zikiungamkono jitihada za serikali kupitia utekelezaji wa miradi na afua mbalimbaliikiwemo miradi ya afya, elimu, mazingira, kilimo , maji, utawala bora, nishatina uwezaji wa jamii.

Ameongeza kwamba utekelezaji wa miradi hiyo umechangia kuboresha utoajihuduma, kuzalisha ajira, kuongeza mapato ya serikali na ukuaji wa uchumikwa ujumla. Dkt. Gwajima amesema Wizara itaendelea kuboresha mazingirawezeshi kwa NGO’s ili ziweze kuisadia jamii kwa kuzingatia mipango, mikakatina vipaumbele vya taifa.

Awali Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali(NaCoNGO) Dkt. Liliani Badi ameiomba serikali kushughulikia changamotombalimbali zinazokabili Mashirika yasiyo ya kiserikali ikiwemo upatikanaji wavibali kwaajili ya utekelezaji wamiradi na afua mbalimbali katika mikoa nahalmashauri mbalimbali, vigezo vya upatikanaji wa misamaha ya kodi pamojachangamoto ya mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa kutozingatiautekelezaji wa takwa la kisheria la kuyajengea uwezo mashirika yasiyo yakiserikali ya ndani ya nchi.

Post a Comment

Previous Post Next Post