Maafisa Ardhi Wahimizwa Kutoa Elimu Ya Matumizi Sahihi Ya Ardhi

Na Mwandishi Wetu, MOROGORO.

 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis amewataka Maafisa Ardhi nchini kutoa elimu ya matumizi borana sahihi ya ardhi ili kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji nchini. 



Ametoa agizo hilo wilayani Mvomero mkoani Morogoro wakati wa uzinduzi waKampeni Maalumu ya ‘Tutunzane Mvomero‘ yenye lengo la kuepushamigogoro ya makundi hayo mawili.

Mhe. Khamis amewataka wananchi kutunza mazingira kwa kuepuka kukatamiti ovyo pamoja na ufugaji usio wa kisasa unaosababisha uharibifu wamazingira.

Amesema kuwa migogoro ya wakulima na wafugaji inasababisha uharibifumkubwa ukiwemo wa mazao, mifugo kuuliwa na kuacha majeraha na vifo kwabinadamu.


“Tupunguze migogoro ya wakulima na wafugaji hebu twendeni tukawafundishe watu wetu namna bora ya kusimamia matumizi ya ardhi ninaamini kila wilaya ina maafisa ardhi, na hili ni agizo la Serikali,“ amesema.

Aidha, kutokana na changamoto ya ukataji miti ovyo, Naibu Waziri Khamis nakwa vile sekta za mazingira, nishati na ardhi ni mtambuka ametoa wito kwamaafisa hao kutoa elimu kwa wananchi kuhusu nishati safi ya kupikia.




“Miti inakatwa sana mimi nimetokea Dar es Salaam nimepita barabarani hasamaeneo ya Morogoro na Pwani unapishana na pikipiki zimepakia mkaa, kamamtakumbuka Rais wetu alifungua mjadala wa nishati safi ya kupikia, maanayake anataka tufanye transormation ya nishati tutoke kwemye kuni na mkaatwende kwenye mishati nyingine ya gesi au umeme,“ amesisitiza.

Pia, Naibu Waziri Khamis amesisitiza wananchi waendelee kupanda miti ikiwani maelekezo ya Serikali na kutekeleza Ilani ya Uchaguzi kuwa kila Halmashauri kupanda miti milioni 1.5 kila mwaka ili kuifanya nchi kuwa ya kijani

Post a Comment

Previous Post Next Post