Kamati Ya Siasa Ya Kata Kilimani Mkoani Dodoma ya Kagua Miradi

 Na Barnabas kisengi Dodoma



Mapema leo tarehe 11 October  2023 viongozi wa kamati ya siasa ya chama cha Mapinduzi  kata ya kilimani  pamoja nawajumbe wa secretariat  ya kata ya kilimani    Wamefanya ziara ya kukwaguwa mradi wa ujenzi wa shule  ya msingi  unatekelezwa katika mtaa wa chinyoyo kata ya kilimani 



Pamoja nakuona kasi  ya ujenzi huo  unavyokwenda  viongozi hao  wamesisitiza ujenzi huo  uzidishe kasi  kulingana na mkataba unavoelekeza  licha yakuwa nachangamoto ndogondogo  ambazo  hazizuii mradi huo  kusimama.


Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi kata ya kilimani Nathani Chibeye amesema ujenzi huo wa shule ya msingi hiyo utakuwa mkombozi kwa kata ya kilimani kwakuwa kata hiyo tangu ipate Uhuru haijawahi kuwa na shule ya msingi jambo ambalo hupelekea watoto wa mitaa nne ya kilimani kusoma katika shule za kata nyingine na kusababisha kutembea umbali mrefu kuitafuta elimu.



"Hata hivi Sasa sisi kama viongozi wa chama cha Mapinduzi kata ya kilimani tunamshukuru SERIKALI YA AWAMU YA SITA INAYOONGOZWA NA RAIS SAMIA SULUHU  HASAN kwa kuweza kutupatia fedha za ujenzi wa shule hii ambayo itakuwa mkombozi kwa wananchi wa kata ya kilimani"amesema chibeye.



Kwa upande wake katibu wa chama cha Mapinduzi kata ya kilimani Rotta Ndimbo ameitaja kamati ya ujenzi na mkandarasi kuhakikisha wanatanguliza uzalendo katika ujenzi wa shule hiyo ili thamani ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi huo zinatumika kama zilivyo kusudiwa.


Ziara hiyo ya viongozi wa chama cha Mapinduzi kata ya kilimani ni mwendelezo wa kugagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali katika kata ya kilimani ili kuhakikisha utekelezaji wa ilani ya chama unafanikiwa

Post a Comment

Previous Post Next Post