Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais
(Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis amesema jumla ya vyeti 190 vya
Tathmini ya Athari kwa Mazingira vimetolewa kwa ajili ya miradi mbalimbali katika
kipindi cha Julai hadi Septemba, 2023.
Amesema hayo wakati
akiwasilisha Taarifa kuhusu Tathmini za
Mazingira Kimkakati pamoja na ufanisi wa Tathmini za Athari kwa Mazingira (TAM) kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji
na Mazingira.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akiwasilisha Taarifa kuhusu Tathmini za Mazingira Kimkakati pamoja na ufanisi wa Tathmini za Athari kwa Mazingira (TAM) kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira leo Oktoba 26, 2023 jijini Dodoma.
Amesema hatua hiyo inaunga mkono azma ya Serikali
kuelekea uchumi wa viwanda hivyo Ofisi imeendelea kupokea miradi mingi kutokana
na ongezeko la wawekezaji katika mbalimbali.
Mhe. Khamis amesema pia Ofisi imechukua hatua mbalimbali na kuweka
mipango ya utekelezaji kwa kupunguza muda wa mchakato wa TAM ambapo miradi hii huhitaji kupata cheti
kilichosainiwa na Waziri mwenye dhamana ya Mazingira.
Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Maji na Mazingira na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wakiwa katika kikao
cha kuwasilisha Taarifa kuhusu Tathmini za
Mazingira Kimkakati pamoja na ufanisi wa Tathmini za Athari kwa Mazingira (TAM) kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji
na Mazingira leo Oktoba 26, 2023 jijini Dodoma.
’’Kwa muongozo huu wa kanuni mpya kwa miradi
yenye ulazima wa kupitia tathmini ya athari kwa mazingira muda umepungua na
kufikia siku 95 kutoka 149 kama ilivyokuwa awali,’’ amesema Naibu Waziri Khamis.
Hali kadhalika Naibu
Waziri amesema kwa
kuzingatia umuhimu wake Miradi ya kimkakati ya Serikali ikiwemo viwanda na
miradi ya kipaumbele ya kilimo inahusika katika vibali hivyo ambacho kinadumu kwa miezi minne ili kuruhusu mchakato wa TAM kwa
mradi husika kukamilika na kupatiwa cheti.
Aidha, ameongeza kuwa Kupunguza Ada na Tozo
za TAM, Kanuni za Ada na Tozo
zimeboreshwa mwaka 2019 na mwaka 2021 ili kupunguza gharama za mapitio ya TAM.
“Ili kuleta maendeleo endelevu, suala la uhifadhi
wa mazingira halina budi kupewa kipaumbele na ili kuhakikisha ufanisi wa miradi
ni vyema kuhuisha masuala ya mazingira katika shughuli za maendeleo hususan
ufanyaji wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira,” amesema.
Hivyo, Ofisi ya Makamu wa Rais itaendelea na
jitihada katika kufanya mapitio ya Kanuni pamoja na miongozo mbalimbali ili
kuboresha tathmini za athari kwa mazingira ikiwemo zile za kisekta ili
kuhakikisha tunakidhi azma ya Serikali ya uchumi wa wiwanda ambao ni endelevu.
Post a Comment