a Pail K, Kahama
Octoba 25,2023
Halmashauri yakabidhi mradi wa ujenzi wa barabara kwa mkandarasi/Chama chaonya watakaokwamisha mradi
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kimesema kuwa hakitamvumilia mtu yeyote au taasisi yeyote itakayo kwamisha mradi wa ujenzi wa barabara za kiwango cha lami unaoanza kutekelezwa hivisasa katika Manispaa hiyo.
Ujenzi huo umefadhiliwa na Benki ya Dunia na unatarajiwa kuanza mapema kwakuwa Octoba 23 tayari Halmashauri ya Manispaa ya Kahama imemkabidhi Mkandarasi rasmi mbele ya Madiwani ambao wamejiridhisha na mkataba uliosainiwa na Jijini Dar ambapo mkandarasi huyo ameoneshwa eneo la Mradi huo atakaotekeleza.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kahama Thomass Muyonga ametoa onyo hilo kwenye kikao maalum cha baraza la Madiwani cha kumtambulisha rasmi mkandarasi wa ujenzi huo pamoja na mkandarasi mshauri wa Mradi ikiwemo kutembelea eneo la mradi unaotarajiwa kuanza muda wowote kuanzia sasa.
“Nasimama hapa kama chama kutamka kuwa kwa mradi kama huu ambao umesubiliwa kwa kipindi kirefu na wananchi na wananchi wetu kwamba hatutavulia kuona kuna mtu ama taasisi yoyote ile inakwamisha mradi huu, badala yake tunapaswa tuungane kwa pamoja kuupokea na kuubariki uanze mara moja ili Manispaa hi ing’are kwa lami,” alisema Muyonga Mwenyekiti wa CCM.
Akizungumza juzi kwenye kikao hicho Mratibu wa Mradi huo Enne Moses alisema kuwa mradi huo inatekelezwa kwa miezio 15 na aliweka bayana gharama halisi ya mradi huo pamoja na utaratibu unaoendelea kwenye mradi kama ulivyogawanywa.
Aidha alifafanua kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama ni moja kati ya Halmashauri 12 zilizopo kwenye awamu ya kwanza (Tier1) ya utekelezaji wa miradi TACTIC.Miradi hii imetengwa katika makundi matatu.
Alisema kuwa utekelezaji wa miradi hiyo ulianza kwa hatua za awali za upembuzi yakinifu, unasanifu na michakato ya manunuzi kwaajili ya kuwapata wataalamu washauri wasimamizi wa mradi (Supervision Consultant) na Mkandarasi (Contractor).
Aliendelea kusema kuwa michakato yote ya awali kwa Package1 imekamilika nan a mikataba kati ya Halmashauri na wataalamu washauri pamoja na Mkandarasi ilisainiwa mnamo tarehe 23,09,2023 mbele ya Waziri wa TAMISEMI Mhe.Mohamed O.Mchengerwa Jijini Dar es Salaam.
Aidha Alisema kuwa Mtaalamu Mshauri wa usimamizi ni Nimeta Consult (T) Limited, mkandarasi wa Package 1 ni Sichuan Road and Bridge (GROUP) Corporation Limited na kubainisha kuwa gharama za mradi thamani yake ni kiasi cha shilingi Bilioni 20,864,094, 611.54.
Pamoja na mambo mengine mratibu huyo wa mradi alisema kuwa miradi itakayotekelezwa kwa huyo mshauri ni pamoja na uboreshwaji wa miundombinu ya barabara eneo la viwanda Zongomera zenye urefu wa kilomita 3, Uboreshaji wa miundombinu ya barabara za mjini kati zenye urefu wa kilomita 11.6.
Aliendelea kusema kuwa maeneo mengine ni ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua eneo la Chelsea-Lyanzungu na shunu Bagomeko yenye urefu wa kilomita 3,Ujenzi wa jingo la mradi lenye ghorofa moja na kwamba miradi hiyo iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
“Kundi la pili inajumuisha miundombinu ya majengo yote yaani ujenzi wa kituo cha mabasi Mbulu, uboreshaji wa soko la Sango Nyasubi, Stendi ndogo ya mabasi Zongomela na soko dogo la Zongomela na kwamba kazi hiyo iko kwenye hatua za ukamilishaji wa nyaraka za zabuni na inategemewa kutangazwa mapema wiki hii,” alisema Mratibu wa Mradi huo Enne Moses.
Aliongeza kuwa kundi la tatu inajumuisha barabara za kilometa 9.6za eneo la viwanda Ummy Mwalimu Zongomela na kwamba kazi hii imefanyiwa usanifu na itatekelezwa kupitia awamu zi
Mkandarasi Mshauri wa mradi huu nimeta consultant LTD imesema imejipanga kuhakikisha ujenzi huu unafanyika kwa kiwango na kukamilika kwa wakatia awamu zitakazofuata kwa kuzingatia upatikanaji wa fedha.
licha ya Madiwani kuupongeza mradi huu na kuahidi kuusimamia kikamilifu ili ulete tija kwa jamii Meya wa Manispaa ya Kahama Yahya Bundala nae alisema mradi huu unapaswa kukamilika ndani ya miezi 15 kama ambavyo wameelezwa na sio vinginevyo.
“Tunachoomba sisi kama madiwani hatuhitaji kuanza kuwashika mashati mradi ukamilike kwa kipindi cha miezi hiyo mitano kama mlivyotueleza na si vinginevyo hali hiyo tutakuwa na majibu yaliyokamilika kwa wananchi wetu,” alisema Meya wa Manispaa.

Post a Comment