Wawakilishi Wa Timu Ya Ofisi Ya Raisi Kwenye Michezo Ya Shimiwi Watakiwa Kurudi Na Ubingwa

 

NAIBU Katibu Mkuu, Ofisi ya Raisi, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Leila Mavika ameiagiza timu ya Ofisi hiyo inayokwenda kushiriki kwenye mashidando ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) mwaka huu kuhakikisha inashindana kwa hali na mali ili kuibuka kidedea.


Katika mashindano hayo ya kusisimua yaliyopangwa kufanyika Mkoani Iringa, Ofisi ya Raisi (Menejimenti ya Utumishi wa Umma) imepeleka wachezaji 46 ambao watashindana katika michezo ya mpira wa miguu, netiboli, baiskeli, pamoja na riadha.

Mwaka 2014, Ofisi hiyo ilishiriki katika mashindano hayo na kufanikiwa kunyakuwa ubingwa, ambapo tangu mwaka huo haikuweza kushiriki tena hadi mwaka huu.

Akizungumza wakati wa ghafla fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwaaga watumishi takribani 46 waliochaguliwa kwa ajili ya kuipeperusha bendera ya Ofisi hiyo katika mashindano ya mwaka huu, Bi. Mavika amewatia shime wawakikilishi hao kuhakikisha wanakwenda kupambana kikamilifu ili kurejesha heshima ya Ofisi hiyo katika mashindano hayo.


“Kwanza kabisa napenda kuwapongeza kwa kuchaguliwa kuiwakilisha Ofisi katika mashindano ya SHIMIWI ya mwaka huu, kwani Ofisi hii inazaidi ya wafanyakazi laki tano hivyo ni lazima mjue mmepewa heshima kubwa sana ya kutuwakilisha,” alisema.

Pamoja na kuwataka washindane kwa ari na kurudi na ubungwa, amewaasa kuonyesha nidhamu ya hali ya juu, ndani na nje ya uwanja.

“Lazime mkumbuke mnakwenda kuiwakilisha Ofisi yenye heshima ya juu sana katika Serikali yetu, hivyo mnapaswa kuwa mfano wa kuigwa na wengine,” aliongeza.



Hata hivyo, amewatia moyo kwamba uongozi wa Ofisi hiyo utasimama bega kwa bega na wachezaji hao katika kipindi chote cha mashindano, na kuwataka wasisite kuwasiliana na uongozi wa Ofisi pale watakapo kutana na changamoto yeyote.

“Ofisi imewekeza sana kwenu, kwa maana ya maandalizi ya timu zetu pamoja na mambo mengine. Hivyo, lengo letu siyo kushindwa na ninatumaini mtatuletea heshima. Kwa niaba ya uongozi wa Ofisi napenda kuwatakia safari njema na mashindano mema,” Bi. Mavika aliongeza wakati wa salamu zake za mwisho za kuwatakia wawakilishi hao baraka.
Kwa upande wake, mwakilishi wa timu hiyo, Charles Shija, alishukuru Ofisi ya Raisi, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa kuwaamini na kuwapatia huduma nzuri katika kipindi chote cha maandalizi.

“Tunajua Ofisi kwa sasa inavipaumbele vingi vya muhimu sana vya kutekeleza, lakini pamoja na hayo mmeona umuhimu wa kuturuhusu na kutusaidia kushiriki katika maishindano ya mwaka huu, tuna ahidi hatuta waangusha,” aliushuruku uongozi wa Ofisi.


Aidha, amesema wachezaji wote wapo katika hali nzuri ya kiafya na wamepata muda mzuri wa kufanya mazoezi chini ya makocha hodari kwa ajili ya siyo kwenda kushiri tu, bali kuirudishia Ofisi heshima ya ubingwa wa mashindano hayo.



Kikosi cha timu zote





Post a Comment

Previous Post Next Post