Tume Ya Madini Yawapiga Msasa Wadau Wa Madini Kwenye Maonesho Ya Madini Geita

 

 _Wadau wapongeza Wizara, Tume ya Madini kwa kufungua fursa katika Sekta ya Madini._ 


Ikiwa ni sehemu ya ushiriki wa Tume ya Madini katika Maonesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini, yanayoendelea katika Uwanja wa Bomba Mbili Mjini Geita, leo wadau wa madini wamepewa elimu kuhusu fursa zilizopo katika Sekta ya Madini pamoja na namna ya upatikanaji wa leseni za madini  kama mkakati wa kufungua fursa kwa wananchi wanaotembelea maonesho hayo.



Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wamepongeza kazi kubwa inayofanywa na Wizara ya Madini na Tume ya Madini kwa kuendelea kutoa elimu kuhusu fursa za uwekezaji katika Sekta ya Madini kama mkakati wa kuvutia ushiriki wa watanzania katika Sekta ya Madini.







Post a Comment

Previous Post Next Post