Na Mwandishi vWetu,Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) Prof. Mkumbukwa Madundo Mtambo amemshukuru Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Awamu ya Sita ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwezesha Shirika hilo kupata vifaa vipya vya maabara ambavyo vitarahisisha utendaji kazi wa shirika.
Prof.Mkumbukwa Madundo Mtambo,
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO )
Prof. Mtambo amezitaja Maabara zilizoweeshwa na Serikali ya Awamu ya Sita hivi karibuni kuwa ni Maabara ya uchunguzi wa kikemia (Analytical Chemistry Laboratory) ambayo inatumika kwa utafiti na uchunguzi wa sampuli mbalimbali kubaini uchafuzi wa mazao na bidhaa za Kilimo kama vile sumu Kuvu (Mycotoxins), Maabara ya Teknolojia ya Chakula (Food Microbiology) ambayo inatumika kwa ajili ya utafiti na uchunguzi wa sampuli za Kibaiolojia, Maabara ya Ngozi na Nguo (Textile and Leather Testing Laboratory) ambayo hutumika kupima kwa utafiti na uchunguzi wa bidhaa za ngozi na nguo kabla na baada ya kuzalishwa.
Dr purificator kiwango(Mtaalam wa MAABARA ya vyakula) akionesha Mashine ya
Atomic absorption Spectrophotometer (AAS) inayotumika kupima kiwango cha Madini kwenye vyakula.
Prof. Mtambo anatumia nafasi kuwakaribisha wadau wote nchini kutumia Maabara za TIRDO hasa katika kipindi hiki ambapo Tanzania ni mwenyeji wa Mkutano wa Kilele cha mifumo ya Chakula Barani Afrika unaotarajia kuanza tarehe 5 hadi 8 Septemba,2023 jijini Dar Es Salaam (AGRF 2023). “Tukiwa na Bidhaa bora zizizohakikiwa na wataalam viwanda vyetu na wafanyabiashara wetu wataweza kutumia soko kubwa la Afrika”-aliongeza Prof. Mtambo.
Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) ni shirika la utafiti na maendeleo ya Viwanda Tanzania lililoanzishwa kwa Sheria ya Bunge namba 5 ya mwaka 1979 na lilianza kufanya shughuli zake tarehe 1 Aprili, 1979. TIRDO ni Shirika la Umma ambalo liko chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara . Jukumu lake ni kusaidia sekta ya viwanda nchini kupitia utafiti na kutoa huduma za kitaalam kusaidia maendeleo ya viwanda.
ReplyForward |



Post a Comment