" Epukeni Rushwa Ujenzi Wa Viwanja Vya Michezo Ya AFCON"" :DC Shekimweri



Na, Anna George 

Dodoma.


Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini,Jabir Shekimweri amesema wale watakao pata zabuni ya kujenga Viwanja vya michezo kwaajili ya mashindano ya AFCON kujiepusa na vitendo vya rushwa kwani athari zake ni nyingi kwa jamii.


Shekimweri amesema hayo leo Septemba 29,2023 Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa mbio za Sepesha rushwa Marathon zinazotarajiwa kufanyika Disemba3 Mwaka huu zenye lengo la kupaza sauti za vijana katika mapambano dhidi ya rushwa.



Pia Amesema ni muhimu kutekeleza adhima ya Rais katika kumpa heshima ambayo amepewa kuwa mwenyeji wa mashindano hayo kwakuepukana na Vitendo hivyo ambavyo havina tija kwa maendeleo ya Taifa.


“Tusipozingatia kanuni na uadilifu katika utendaji kazi na tunaweza kusababisha kuwa na Wataalam wasio na sifa na kuleta hasara kwa Taifa,”


Kwa upande wake  Katibu wa Chama cha riadha Mkoa wa Dodoma Bw.Robert Mabonye amepongeza ujio wa mbio hizo za sepesha rushwa Marathon kwani ni fursa kwa wakazi wa Dodoma na Watanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki.


“Ni muhimu kwa wana Dodoma Sasa na Watanzania kujitokeza Kushiriki kwani baadae kutakuwa na zawadi mbalimbali,”


Awali Katibu Mtendaji wa Sepesha rushwa,Kubega Dominic amesema ""Sepesha rushwa Marathon ni mbio zinazoandaliwa na vijana wa kupinga rushwa huku akieleza malengo mbalimbali""

Post a Comment

Previous Post Next Post